SHARE

NA JESSCA NANGAWE
MWANADADA Isha Mashauzi anayefanya vyema kwenye muziki wa taarabu amefunguka kuwa kwa sasa ni Somo mzuri sana wa kuwafunda Wanawake na Wanaume pindi wanapotaka kuingia kwenye Ndoa.
Akizungumza na DIMBA, Isha alisema kwa wale wanawake wanaotaka kuingia kwenye ndoa na hawana elimu yoyote katika hilo wanaweza kumuona ili aweze kuwapa elimu kidogo kabla ya kufanya maamuzi hayo.
“Sio kwamba najua kila kitu kwenye ndoa, hapana, hiki kidogo nilichonacho napenda kujifunza na wenzangu, nimeshuhudia ndoa nyingi zinavunjika lakini pia wengi wanaingia bila kuwa na taswira ya nini wanakwenda kukutana nacho”alisema mwanadada huyo.
Hata hivyo ameongeza kuwa wanawake wasiwe waoga kufanya maamuzi ya kuingia kwenye ndoa pindi wanapopata nafasi hiyo wakihofia usaliti kwani kunawasaidia kuepuka mambo mengi ikiwemo watoto kukataliwa na baba zao.
@@@@@@@@@@@@@

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here