SHARE

ZIPO taarifa zinazoendelea kwa sasa kuwa uongozi wa klabu ya Simba upo katika mipango ya kumrudisha mshambuliaji wao wa zamani, Emanuel Okwi ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya SonderjyskE inayoshiriki Ligi Kuu nchini Denmark.

Mchezaji huyo raia wa Uganda, kwa sasa anaonekana hana nafasi ya kucheza kwenye klabu yake hiyo mpya aliyojiunga nayo Julai mwaka huu.

Taarifa za kurejea kwa mshambuliaji huyu zilianza kuenea kwa takribani miezi miwili sasa, huku kukiwa na habari kuwa klabu yake ya sasa inahitaji dau la Sh milioni 220 ili waweze kumwachia.

Hata hivyo, uongozi wa Simba bado haujaweka wazi suala hilo kama ni kweli au la, lakini upo msemo wa Kiswahili unaosema ‘lisemwalo lipo kama halipo basi laja’.

Lakini pia kwa upande wa Yanga zipo taarifa kuwa wapo kwenye harakati za kuinasa saini ya straika wa zamani wa Azam FC, Kipre Tchetche ambaye kwa sasa anacheza kwenye klabu ya Al-Nahda Al-Buraimi ya Oman.

Kipre alisaini kuitumikia timu hiyo akiwa bado ana mkataba na Azam wa mwaka mmoja, lakini hata hivyo bado anahusishwa na kujiunga na Yanga.

Taarifa za mchezaji huyo kujiunga na Yanga zilianza kuenea mapema kabla hata ya kusaini nchini Oman na bado inasemekana uongozi wa Wanajangwani hao upo kwenye rada za kumnasa mchezaji huyo.

Ukiwa kama mdau wa soka nchini, unadhani kuwa timu za Simba na Yanga bado zinawahitaji wachezaji hao kwa sasa?

Simba inafanya vizuri kwenye michuano ya Ligi Kuu Bara tangu ilipoanza kutimua vumbi Agosti 20, mwaka huu na kufanikiwa kuongoza ligi ikiwa na pointi 35, huku mchezaji wake, Shiza Kichuya, akiongoza kwenye orodha ya wafungaji akiwa na mabao 9.

Yanga pia inafanya vema kwenye michuano hiyo ikiwa katika nafasi ya pili kwenye msimano baada ya kujikusanyia pointi 30, huku wachezaji wake kadhaa wakiwa kwenye orodha ya wafungaji bora.

Kwa kuviangalia vikosi vya timu hizo zote mbili unadhani wachezaji hao, Okwi na Tchetche, wanayo nafasi ya kucheza kwenye timu hizo au zinaonekana kuwahitaji?

Tuma maoni yako kwa ujumbe mfupi wa maneno ukianzia na jina lako na mahala ulipo.

 

*****

Mada ya wiki iliyopita

Wiki iliyopita kulikuwa na mada kuwa kutokana na maoni ya wasomaji pamoja na wadau wa soka nchini, wanapangaje kikosi cha kwanza cha Manchester United.

Wadau wengi walitoa maoni yao juu ya kikosi hicho na wengine kujaribu kupanga ni namna gani kikosi cha kwanza cha timu hiyo kinatakiwa kiwe.

 

****

Naitwa, Jafari Abdalla wa Dar, kikosi changu ni David de Gea, Antonio Valencia, Eric Bailly, Chris Smalling, Luke Shaw, Ander Herrera, Michael Carrick, Paul Pogba, Henrikh Mkhitaryan, Marcus Rashford, Anthony Martial.

 

****

Naitwa, Juma Jamali wa Mbeya, David de Gea, Antonio Valencia, Daley Blind, Chris Smalling, Eric Baily, Morgan Schneiderlin, Juan Mata, Paul Pogba, Zltan Ibrahimovic, Henrikh Mkhitaryan, Marcus Rashford.

 

****

Mimi ni Mbaraka Yusuph wa Tanga, kikosi cha kwanza kinapaswa kuwa ni David de Gea, Antonio Valencia, Daley Blind, Chris Smalling, Eric Baily, Ander Herrera, Marcus Rashford, Juan Mata, Zltan Ibrahimovic, Anthony Martial.

 

****

Jina langu ni David Marcus wa Arusha, kikosi cha kwanza kinapaswa kuwa ni David de Gea, Antonio Valencia, Luke Shaw, Eric Bailly, Chris Smalling, Ander Herrera, Jesse Lingard, Michael Carrick, Zltan Ibrahimovic, Paul Pogba, Marcus Rashford.

 

****

Naitwa, Joseph Amos wa Tabora, kikosi cha kwanza ni David de Gea, Antonio Valencia, Luke Shaw, Eric Bailly, Chris Smalling, Ander Herrera, Paul Pogba, Zltan Ibrahimovic, Anthony Martial, Marcus Rashford.

 

****

Mimi ni Paul Kambangwa wa Iringa, kocha anapaswa kupanga kikosi hiki, David de Gea, Antonio Valencia, Matteo Darmian, Marcos Rojo, Michael Carrick, Memphis Depay, Paul Pogba, Zltan Ibrahimovic, Wayne Rooney, Marcus Rashford.

 

***

Naitwa, Khalid Hassan wa Dar, kikosi cha Man Utd ni David de Gea, Matteo Darmian, Marcos Rojo, Phil Jones, Delay Blind, Michael Carrick, Ashley Young, Ander Herrera, Zltan Ibrahimovic, Wayne Rooney, Paul Pogba.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here