SHARE

NA GLORY MLAY

KLABU  tano za Judo Tanzania zimeondoka jana kuelekea katika mashindano ya kitaifa ya klabu za mchezo huo(Budokan Cup) yatakayofanyika leo Visiwani Zanzibar.

Mashindano hayo yatawashirikisha wachezaji kutoka Pemba, Unguja, Tanzania bara na Afrika Kusini wakiwamo wanawake na wanaume.

Akizungumza na DIMBA jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Judo nchini (JATA) Innocent Malya,  alisema mashindano hayo yatasaidia kuweza kupata timu bora ya taifa ambayo itaiwakilisha nchi katika mashindano ya Afrika Mashariki yatakayofanyika Zanzibar hapo mwakani.

“ Mashindano hayo yatakuwa na upinzani mkali kutokana na kuwepo wacheza judo kutoka sehemu mbalimbali, tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi ili kuweza kuwaunga mkono wenzetu,”alisema.

Malya alisema, mashindano ya kitaifa yaliyomalizika hivi karibuni yameweza kuwapatia vipaji vipya ambavyo vitaweza kuitangaza nchi katika mashindano mbalimbali ya yakiwamo hayo ya Zanzibar

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here