SHARE

ABDULAH MKEYENGE

NIMEKIONA kikosi cha Simba jana dhidi ya Power Dyanamo. Ahsante kwa ushindi mnono na shukrani kwa mabao ya Meddie Kagere yaliyoipa Simba ushindi wa 3-1 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Namuona Kagere akiibuka tena mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara. Yule Msudan Sharaf Eldin Shabib,ni back-up ya Kotei au Niyonzima? Kama Kotei Simba irudi sokoni kumtafuta mbadala wake.

Yule Mbrazil namba 4 mgongoni ni kama Mu- ingereza. Anachokifanya ni kutimiza majukumu yake kiwanjani. Hakai nao. Hana mbwembwe. Anapiga moja anaachia. Anajiweka sehemu salama apasiwe.

Yule beki wa kati Mbrazil natamani kumuona tena na tena. Kahata ni Niyonzima mwenye rasta. Chama ndio mfalme mpya Msimbazi. Vipi Deo Kanda jezi imemtosha?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here