SHARE

NA WINFRIDA MTOI

SERIKALI ya Rwanda, imeongeza muda kwa wananchi wake kukaa ndani ya nyumba pasipo kutoka nje na mipaka kuendelea kufungwa hadi Aprili 30 mwaka huu, hivyo kuondoa matumaini ya mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, kurejea nchini kwasasa.

Awali baada ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona kuingia nchini humo, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, alitoa agizo la wananchi wake kukaa ndani ya nyumba ‘lockdown’ kwa siku 14 iliyokuwa inatarajiwa kuisha Aprili 4 lakini akaongea siku zingine 14 ambayo zilitarajiwa kumalizika leo.

Hata hivyo, kutokana na maambukizi kuzidi kuongezeka, serikali ya Rwanda imeamua kuongeza siku za watu kuendelea kukaa ndani na mipaka kufungwa hadi Aprili 30 mwaka huu lengo likiwa ni kudhibiti maambukizi.

Kitendo cha mipaka kufungwa na watu kutoruhisiwa kutoka au kuingia ndani ya nchi hiyo, kutamfanya Kagere ashindwe kuondoka, ukizingatia na Tanzania nayo imefunga mipaka.

Hivi karibuni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Senzo Mbatha, alisema angetamani nyota wake waliopo nje ya nchi wapate ruhusa ya kurejea nchini mapema ili waweze kukaa karantini kwa siku 14.

Tofauti na Kagere, wachezaji wengine wa Simba waliokwama katika nchi zao kutokana na janga hili la corona ni Clatous Chama (Zambia), Luis Miquissone (Msumbiji), Francis Kahata (Kenya) na Sharaf Shiboub (Sudan).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here