SHARE

MANCHESTER, England


KAMA Manchester United wanahitaji kuwa mabingwa wa Ligi Kuu England msimu ujao, basi wameshauriwa kuifukuzia saini ya straika wa Tottenham, Harry Kane ili kuongeza nguvu katika kikosi chao.

Mchambuzi wa soka, Paul Merson, amempa habari hiyo kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer kuwa kikosi chake kinahitaji straika mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao kuliko kuendelea na Anthony Martial ambaye amekuwa na vipindi vya kushuka na kupanda ndani ya timu hiyo.

“Namuona Kane kama mchezaji sahihi wa kuongoza safu ya ushambuliaji ya Manchester United, kama Solskjaer anahitaji kushinda na Liverpool au Manchester City, basi amsajili straika huyo wa Tottenham.

“Martial ni mchezaji mzuri, lakini anapitia vipindi tofauti vya kushuka na kupanda kiwango, Mason Greenwood bado kijana mdogo ambaye anatakiwa kujifunza taratibu,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here