SHARE

NA EZEKIEL TENDWA

YANGA inatarajiwa kutangaza jina la Katibu Mkuu mpya kesho ambaye atavaa viatu vya Omar Kaaya aliyeachana na kazi hiyo na nafasi yake kukaimiwa na Dismas Ten.

Nafasi hiyo ya katibu awali ilikuwa ikishikiliwa na Charles Boniface Mkwassa, lakini akajiweka pembeni ndipo Kaaya akakabidhiwa jukumu hili na sasa Dismas amekaimu kwa muda.

Taarifa kutoka Yanga zinadai kuwa, tayari vikao vya Kamati ya Utendaji chini ya mwenyekiti wa Klabu hiyo Dk.Mshindo Msola vimeshamalizika na kilichobakia ni kuweka jina la bosi huyo mpya hadharani.

“Kila kitu kipo tayari, nadhani Jumatatu Wanayanga watatangaziwa jina la katibu wao mkuu ambaye ataungana na viongozi wengine kuhakikisha klabu inasonga mbele.

“Kitu kilichoziangatiwa katika suala hilo, kwanza ni uchapakazi wa mhusika, nidhamu ya kazi lakini pia mtu ambaye ana ushirikiano na wenzake, kwani bila hivyo mambo yatakwenda ‘shaghalabaghaba’, alisema kigogo mmoja wa Yanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here