SHARE

NA WINFRIDA MTOI

KOCHA mpya wa Yanga, Mrundi Cedric Kaze, anatarajiwa kutua kesho kuanza kazi ya kukinoa kikosi hicho kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kaze anatua Jangwani kuchukua nafasi ya Mseribia, Zlatko Krmpotic, aliyefukuzwa baada ya uongozi kutoridhishwa na mwenendo wa kikosi hicho.

Kocha huyo raia wa Burundi, anawasili akiwa tayari ameisoma timu hiyo na ndiye aliyeshauri kusajiliwa kwa kiungo wa Vital’O, Said Ntibazonkiza.

Ntibazonkiza alisajiliwa na Wanajangwani hao baada ya kumaliza mechi ya kirafiki juzi kati ya Burundi na Taifa Stars na ndiye aliyefunga bao la pekee la timu yake iliyoshinda 1-0 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Inadaiwa kuwa usajili huo ni kutokana na mifumo mitatu anayokuja nayo Kaze katika kuhakikisha anakisuka upya kikosi cha Yanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here