SHARE

NA WINFRIDA MTOI

KATIKA suala la ulinzi wa pembeni, Yanga imeshamaliza kazi kutokana na majembe mawili waliyoyasajili, Kibwana Shomari, mlinzi wa kulia na Yassin Mustafa upande wa kushoto kuwa katika kiwango kizuri.

Wachezaji hao wamedhihirisha kuwa Yanga, haijafanya makosa kutokana na kiwango walichokionesha katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Shomari aliyesajiliwa na Yanga kutoka Mtibwa Sugar, amekuwa akihakikisha anaziba pengo la Juma Abdul aliyeachwa akisaidiana na Paul Godfrey ‘Boxer’.

Kwa upande wa Mustafa yeye ameonesha wazi kuwa yuko fiti kwa kuondoa tatizo la muda mrefu la beki wa kushoto ambalo baadhi ya wachezaji waliosajiliwa msimu uliopita walishindwa.

Hata hivyo benchi la ufundi ndilo litakuwa na jukumu la kuchagua ni mchezaji gani anaweza kuendana na mfumo na kasi ya Wanajangwani hao wanaopigania kurudisha heshima ya kwa kutwaa ubingwa msimu ujao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here