SHARE

Jassca Nangawe

KUREJEA kwa Winga wa Simba Ramadhan Kichuya huenda ikawa furaha kwa straika wa kikosi hicho Meddie Kagere kurejesha kasi yake ya kupachika mabao msimu huu.

Kagere ambaye tayari ameshafunga mabao 10 mpaka sasa akiongoza nafasi hiyo, ameonekana kupunguza kasi katika mechi za hivi karibuni ambapo hajaweza kutupia mabao kama alivyozoeleka.

Kichuya amerejea kwa mara nyingine kukitumikia kikosi hicho na ameahidi kushirikiana vyema na wachezaji wenzake kuhakikisha anaisaidia Simba kuvuna matokeo mazuri ikiwemo kutetea ubingwa wao.

Akizungumza na Dimba Kichuya alisema, amekuja Simba kuhakikisha anaendeleza pale alipoishia lakini kikubwa ni kushirikiana vyema na wenzake kwa kila hatua ili kuipa timu hiyo matokeo mazuri.

Alisema amekuwa akiifuatilia timu hiyo kwa kipindi chote alichokua hayupo na anatambua bado ni timu inavyofanya vizuri, hivyo ni matarajio yake itazidi kupambana kwa kila mchezo ulio mbele yao.

Hii itakua neema kwa mpachika mabao wa timu hiyo Kagere ambaye ushirikiano wao huenda ukazaa matunda na kurejesha kasi yake ya mabao ambayo imeonekana kupungua kwa kasi zaidi kwa siku za hivi karibuni.

Hii inatokana na Kichuya kuwa na uwezo mkubwa wa kupiga pasi za mwisho ambazo mpachika mabao kama Kagere itakuwa rahisi kumalizia.

Kichuya amerejea Simba akitoka nchini Misri ambapo alikua akicheza soka la kulipwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here