SHARE
Thomas Partey

MADRID, Hispania 

ATLETICO Madrid wanaimani ya kumpa mkataba mpya kiungo wao mkabaji, Thomas Partey, ambaye yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaowaniwa na kocha wa Arsenal, Mikel Arteta. 

Katika misimu ya hivi karibuni, Arsenal imekuwa ikiruhusu mabao na hawaonyeshi kupambana ndiyo maana Arteta anamwania Mghana huo akiamini ataibadili timu yake baada ya kun’ara kwa misimu mitatu chini ya Diego Simeone.

Kabla ya soka la Ulaya kusimamishwa kutokana na janga la virusi vya corona, Partey alikuwa nyota wa mchezo katika mchezo wa nyumbani na ugenini dhidi ya Liverpool katika hatua ya 16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya. 

Kuna kipengele cha pauni za Uingereza milioni 43 (shilingi bilioni 107) kinachoruhusu Partey kuachiwa na ripoti kutoka Italia zinadai wiki iliyopita Arsenal waliwasilisha ofa ya kiasi hicho. 

Lakini Atletico wanahaha kumfunga na mkataba mpya mchezaji huyo wa miaka 26 huku mazungumzo yakiwa yameshaanza kitu ambacho kitafanya dau ya kipengele hicho kupanda hata kama mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2023. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here