SHARE

MERSEYSIDE, England

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amemvaa mwenzake wa Chelsea, Frank Lampard, akimwambia ana safari ndefu ya kujifunza katika taalamu hiyo ya kufundisha soka.

Katika mchezo wao wa hivi karibuni, ambao ulimalizika kwa Chelsea kuchapwa mabao 5-3, Lampard alikwaruzana na Klopp na msadizi wake, Pep Lijnders.

Kwa Lampard kuwatolea maneno machafu Liverpool baada ya mechi hiyo ya nusu fainali ya Kombe la FA, Klopp alijibu: “Kusema vile baada ya mechi, sidhani kama ni sawa. Frank anatakiwa kujifunza, ana muda mwingi sana wa kujifunza kwa sababu bado ni kocha mchanga…”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here