SHARE

GLORY MLAY

KOCHA Mkuu wa Simba Queens, Musa Hassan Mgosi, amesema kutokana na programu ya mazoezi wanazoendelea nazo anaamini timu hiyo haitoshikika msimu ujao.

Akizungumza na DIMBA Jumatano,Mgosi alisema,kila mchezaji ameahidi makubwa kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara.
Alisema, wachezaji wote wameonyesha kujituma zaidi mazoezini ili kumuonesha uwezo walionao kuelekea msimu mpya kwani wanahitaji kuchukua ubingwa.

Alisema pia wanampando wa kuingia darasani kupewa mafunzo mbalimbali ili kuwaongezea uelewa wachezaji wake ikiwemo elimu ya saikolojia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here