SHARE

                 Lulu Ringo, Dar es Salaam

Kikosi cha Simba kimeendelea kujifua katika viwanja vya Boko Veterani kuelekea mchezo wao dhidi ya Stand United utakaopigwa Octoba 21, katika uwanja wa Taifa.

Kocha wa Simba Patrick Aussems ameonekana akikinoa kikosi hicho hasa katika upande wa ushambuliaji na kiungo mazoezi yenye taswira ya kutafuta matokeo zaidi katika mechi hiyo.

Ikumbukwe Simba imepoteza mchezo mmoja na kutoa sare mbili ikiwa na jumla ya alama 14 sawa na Mbao Fc na Jkt Tanzania Simba wao wakishikilia nafasi ya tano katika msimamo wakitofautiana idadi ya mabao ya kufungwa na Kufunga lakini pia Simba ipo nyuma mchezo mmoja.

Baadhi ya wachezaji waliokua wakifanya mazoezi hayo ambao ndio walionekana watatoa kikosi kitakachoikabili Stand ni  Magolikipa Aish Manula na Deogratius Munishi,  Hassan Dilunga, Adam Salamba, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Meddie Kagere, Said Ndemla, Asante Kwasi, Mohamed Rashid, Mohamed Hussein, Mzamiru Yassin, Shiza Kichuya, James Kotei, Marcel Kaheza na  Nicolus Gyan.

Aidha wachezaji waliokosekana katika mchezo huo ni Mnyarwanda Haruna Niyonzima, Mzambia Clatous Chama Niyonzima na Mganda Emanuel Okwi, wachezaji majeruhi ni Jonas Mkude aliyeumia akiwa kambini na timu ya Taifa hata hivyo alikua ni mmoja kati ya wachezaji waliofanya mazoezi lakini mazoezi yake yalikua mepesi tofauti na yale walifanya wengine.

Simba itaikabili Stand ikiwa na wachezaji wake muhimu Hassan Dilunga na Mzamiru Yassin waliorejea kutoka majeruhi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here