SHARE

Mjue Jay Jay Okocha (21)

NA BADI MCHOMOLO

HII ni wiki ya mwisho kabla ya kuumaliza mwaka 2019. Habari gani msomaji wa safu hii pendwa ambayo imekuwa ikiyaanika maisha ya gwiji wa soka kutoka nchini Nigeria, ambaye aliitikisa dunia, Augustine Azuka kwa jina la kuzaliwa, lakini anajulikana kwa jina la Jay Jay Okocha.

Aliwashangaza wazungu kwa aina ya mpira aliokuwa anacheza na aliwaaminisha kuwa Afrika kuna wachezaji wenye uwezo wa kushangaza dunia.

Wiki iliopita tuliona jinsi mchezaji huyo alivyowaachia PSG zawadi ya nyota wa soka kutoka nchini Brazil, Ronaldinho Gaucho. Kwa kukukumbusha ni kwamba, Okocha wakati anaondoka ndani ya klabu ya PSG mwaka 2002, alimuacha Gaucho, hivyo nafasi yake ikawa inachukuliwa na mchezaji huyo.

Kabla ya Okocha kuondoka alikua rafiki wa karibu wa Gaucho, hivyo alikuwa anamfundisha mambo mengi baada ya mazoezi pamoja na mechi, mafunzo hayo yalikuwa yanamfanya Gaucho kuwa mkomavu na muelevu jambo ambalo lilikuwa kama zawadi kwa mashabiki wa PSG baada ya Okocha kwenye kujiunga na Bolton Wanderers FC.

…leo tunaangalia ni kweli kuwa nyota wa zamani wa timu ya Arsenal, Alex Iwobi ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Everton ni mjomba wa Okocha?

Jibu ni rahisi tu kwamba ndio mjomba yake. Hata suala la Iwobi kucheza mpira limetokana na Okocha, inawezekana kama hasingekuwa mmoja kutoka kwenye fainali hiyo basi leo hii tusingemjua Iwobi kwenye ramani ya soka.

Undugu wa Okocha na Iwobi umetokana na mama wa Iwobi ni dada wa Okocha, huko Okocha akiwa na kaka wawili na dada mmoja ambaye ndio mama wa Iwobi.

Iwobi alizaliwa mwaka 1996, hivyo wakati huo Okocha yupo kwenye ubora wake wa kucheza soka. Wakati Iwobi anakuwa Okocha walikuwa anampenda sana hivyo wakati wa likizo alikuwa anapenda kukaa naye pamoja.

Iwobi hakuwa na lengo la kucheza mpira, lakini kutokana na ukaribu wake na Okocha alijikuta akipenda kucheza soka hasa kutokana na kumuona mjomba wake kwenye runinga.

Inasemekana kuwa, Okocha alikuwa na lengo la kutaka kumuachia urithi wa soka ili jina la familia hiyo lizidi kuwa kubwa mara baada ya yeye kustaafu.

“Ni kweli Iwobi ni mtoto wa dada yangu, hakuwa mtu wa kupenda mpira sana, lakini mimi na mama yake tumepambana kwa kiasi kikubwa kumfanya apende mchezo huo, ninaamini tumefanikiwa kwa kuwa tayari amecheza Arsenal na sasa anacheza Everton.

“Lengo langu lilikuwa aje kuwa mmoja kati ya mastaa ndani ya Nigeria pamoja na duniani kote, lakini ushindani wa sasa ni mkubwa hivyo anakutana na changamoto ya hali ya juu, ila kwa upande wake anaendelea kufanya vizuri.

“Kila nikikutana naye nimekuwa nikipambana hadi sasa kumpa mbinu mbalimbali za kufanya ili awe bora zaidi ya hapo alipo, naweza kusema mimi ni mmoja kati ya watu wake wa karibu kwa ushauri, dada anajivunia kuwa na kijana huyo na mimi ninajivunia,” alisema Okocha.

Msomaji nikutakie heri ya Krismasi na Mwaka Mpya. Tukutane Januari mwakani.

@@@@@@@

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here