SHARE

NA JESSCA NANGAWE

STAA wa Bongofleva Faustina Charles maarufu ‘Nandy’ amesema miongoni mwa watu waliomfanya kupenda mambo ya urembo ni pamoja na mwanamitindo maarufu duniani Kylie Jenner.

Nandy mapema wiki hii amezindua duka lake la Nandy Bridal litakalokua likijishughulisha na mambo ya kupamba maharusi na kuuza bidhaa za urembo amesema, ilimchukua muda mrefu kutimiza ndoto hiyo.

“Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa hili, haikuwa na ndoto ya muda mfupi, nadhani ilitangulia hata mambo yangu ya muziki, nilipenda urembo tangu nikiwa mdogo na moja ya watu ambao wamenifanya leo kuwa hapa ni pamoja na mwanamitindo Kylie Jenner”alisema Nandy.

Nandy alisema uwezo wa Kylie Jenner licha ya umri wake kuwa mdogo ni kujituma na kupambana kuhakikisha anatimiza  yote yaliyo kwenye ndoto zake.

Staa huyo ameongeza kuwa kwa sasa shughuli zake zote zitakuwa zikifanyika ndani ya ofisi hizo mpya ambazo zipo maeneo ya Mbezi, Dar es salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here