SHARE

ROME, Italia 

LAZIO inapanga kuimarisha kikosi chake msimu unaokuja kwa kumnyakua straika wa Wolverhampton Wanderers, Diogo Jota, hayo ni kwa mujibu wa gazeti la A Bola.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno anaweza kujiunga na klabu hiyo ya Serie A endapo Biancoceleste kama inavyofahamika itafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. 

Lazio kwasasa ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikizidiwa pointi moja na vinara Juventus kabla ya msimu kusimamishwa kutokana na virusi vya corona.

Jota ambaye ana umri wa miaka 23, ana mkataba na Wolves unaomalizika June 2022 huku tayari akiwa amefunga mabao sita na kutengeneza saba katika mechi 25 za ligi. 

Msimu uliopita, Lazio iliwauzia Wolves wachezaji wawili kutoka Ureno; Pedro Neto na Bruno Jordao, na kwa mujibu wa A Bola, uhusiano mzuri kati ya klabu hizo mbili na wakala wa Jota, Jorge Mendes, unaweza ukarahisisha dili hilo. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here