SHARE

NA TIMA SIKILO

STRAIKA wa Yanga, Heritier Makambo, ameichimba mkwara Azam FC baada ya kusema atahakikisha anawafunga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Jumatatu inayokuja.

Timu hizo hazijakutana mchezo wowote msimu huu na Jumatatu kila moja atataka kuhakikisha anapata pointi tatu ambazo zinaweza kuwapeleka mbele zaidi wakati huu ligi ikielekea ukingoni.

Makambo ambaye anashika nafasi ya pili kwenye ufungaji akiwa na mabao 15, amesema ataifunga Azam FC ili kuongeza akaunti yake na kuwapiga bao waliopo mbele yake.

Meddie Kagere wa Simba na Salim Aiyee ndio wanaoongoza kila mmoja akiwa na mabao 16 kitu ambacho kinaonekana kumkera Makambo na kutamba kwamba ataiamua mechi na Azam mapema tu.

Makambo ameliambia DIMBA Jumatano kuwa, ana uhakika wa kufunga katika mchezo huo kwani lengo lake ni kuona Yanga ikiibuka na ushindi lakini pia yeye akiongeza idadi ya mabao.

Wanajangwani hao wapo kileleni mwa msimamo wakiwa na pointi 74 baada ya kucheza michezo 32 wakifuatiwa na Azam wenye pointi 66 wakicheza michezo 32, huku Mnyama Simba akizidi kuwapumulia akifikisha pointi 63 baada ya kushinda mchezo wa jana dhidi ya Alliance.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here