SHARE

LONDON, England


MKUU wa benchi la ufundi la Liverpool, Jurgen Klopp, ameinyakua tuzo ya Chama cha Makocha wa ligi Kuu ya England (LMA) kwa mafanikio yake msimu huu uliokwisha hivi karibuni.

Klopp aliipa Liverpool taji la Ligi Kuu, ikiwa ni baada ya timu hiyo kulisubiri kwa miaka 30, mafanikio yaliyotanguliwa na ubingwa wa Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.

Aliyetangaza Klopp kuwa ndiye mshindi ni kocha wa zamani wa Manchester United, Alex Ferguson. “Tunazungumzia Leeds United kurudi Ligi Kuu baada ya miaka 16 lakini ubingwa wa Liverpool baada ya miaka 30 ni jambo la kusisimua,” alisema Ferguson.

Aidha, Klopp naye alizungumza baada ya kupewa tuzo hiyo, akisema amefurahia na si yake, bali kwa kila aliyekuwa kwenye benchi la ufundi la Liverpool.

Tyson kumpa Mayweather bil. 160/-

LOS ANGELES, Marekani

BONDIA Floyd Mayweather ataingiza Pauni milioni 54 (zaidi ya Sh bil. 160 za Tanzania) endapo atazichapa na mkongwe Mike Tyson katika pambano la hisani.

Hili ni dili jingine kubwa kwa Mayweather, ikikumbukwa kuwa mwaka juzi alilipwa Pauni milioni saba kwa dakika mbili tu alizotumia ulingoni dhidi ya Tenshin Nasukawa mjini Tokyo, China.

Tyson, akiwa na umri wa miaka 54 kwa sasa, atazichapa na Roy Jones Jr (51) katika pambabano lililotajwa kuwa ni la raundi nane.

Mayweather alitangaza rasmi kustaafu ndondi za kulipwa mwaka 2017 baada ya kumtandika mchezo wa ngumi na mateke, Conor McGregor

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here