SHARE

ATTERIDGEVILLE, Afrika Kusini

TIMU ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imefuza ubingwa wa Afrika ngazi ya klabu baada ya kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani kwa kupata ushindi mnono wa mabao 3-0 ilipoikaribisha Zamalek ya Misri.

Mchezo huo ambao ulikuwa mgumu kwa timu zote mbili ulifanyika kwenye Uwanja wa Lucas Moripe uliopo, Atteridgeville mjini Pretoria na ulikuwa mchezo wa fainali ya kwanza.

Mabao ya Mamelodi yalifungwa na Anthony Laffor, Tebogo Langerman na Percy Tau akifunga bao la mwisho na kuwafanya wenyeji kutoka kifua mbele wakisubiri fainali ya mwisho ambayo itapigwa  katika mji wa Alexandra,  katika Uwanja wa Borg El Arab Jumapili ijayo.

Licha ya Zamalek kuonekana kuwa imara na wenye kujipanga vyema huku wakiwa wanacheza mchezo wa kujihami zaidi lakini walijikuta katika wakati mgumu baada ya kufungwa bao la kwanza katika dakika ya 31 kipindi cha kwanza lililofungwa na Anthony Laffor.

Baada ya bao hilo Zamalek waliendelea kucheza kwa tahadhari na kujilinda zaidi huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza kulingana na nafasi wanayopata lakini walijikuta wakifungwa bao la pili katika dakika 40 kipindi cha kwanza lililofungwa na Tebogo Langerman.

Kutokana na mabao hayo ya haraka haraka, iliwalazimu Zamalek kucheza kwa tahadhari zaidi lakini wakiendelea kufanya mashambulizi ya kushtukiza  hali iliyowapa nafasi wenyeji kucheza kwa kujiamini zaidi na kufanya matokeo kubakia 2-0 hadi dakika 45 za kwanza.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kiucheza kwa tahadhari ambapo Mamelodi walilazimika kuwa makini zaidi na kushambuliana kwa mazamui lakini wenyeji waliweza kupata bao la tatu lililofungwa na Percy Tau katika dakika ya 46 ikiwa ni dakika moja tu baada ya kupindi cha pili kuanza.

Kutokana na matokeo hayo, Mamelodi inahitaji sare ya aina yoyote ili kuweza kutwaa ubingwa huo kwani ili kupoteza italazimika Zamalek ambao watakuwa wenyeji kushinda si chini ya mabao 4-0 au zaidi.

Timu hizi zimekutana mara tatu kwa mwaka huu pekee ambapo, mechi ya kwanza Julai 17 mwaka huu kwenye michuano hiyo hatua ya makundi Zalek ikiwa nyumbani ilifungwa mabao 2-1, mchezo wa pili ikafungwa ugenini bao 1-0 na hatua ya fainali oktoka 15 mwaka huu Mamelodi ilishinda mabao 3-0 ikiwa uwanja wake wa nyumbani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here