SHARE

MANCHESTER, England


KABLA ya mchezo wao dhidi ya mabingwa wa La Liga, Real Madrid, wakali wa jijini Manchester, Manchester City, wamepanga kucheza mechi ya kirafiki ili kujiweka sawa.

Man City walioambulia nafasi ya pili msimu wa Ligi Kuu ya England uliokwisha hivi karibuni, watawakaribisha Madrid mwezi ujao (Agosti 7), ikiwa ni mechi ya marudiano ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mkurugenzi wao, Txiki Begiristain, anasaka timu ya kujipima nayo kwa kuwa kikosi chake hakitakuwa na mechi yoyote hadi kufikia siku hiyo ya kuikabili Madrid.

Dhidi ya Madrid, Man City watashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa katika Uwanja wa Santiago Bernabeu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here