SHARE

NA JESSCA NANGAWE

MSANII wa Hip Pop Stamina amesema anatarajia kupa mtoto wa kiume wakati wowote na atampa jina la staa wa soka dunia Lionel Messi.

Stamina amesema wakati wowote anatarajia kupanua familia yake kwa kupata mtoto wa kwanza ambaye atakua wa kiume na tayari wamemwandalia jina la Lionel kutokana na mapenzi yake kwa staa huyo.

Akizungumza na DIMBA,Stamina alisema, sababu kubwa ya kumwita mwanaye jina la Lionel ni kuendeleza mapenzi yake kwa mwanasoka huyo ambaye amekua akimkubali kwa kiasi kikubwa.
“Tunatarajia kupata

mtoto wakati wowote, na sasa teknolojia imepanuka, natarajia kupata mtoto wa kiume ambaye tumeshamwandalia jina la Messi, nimefanya hivyo kutokana na mapenzi yangu kwa mwansoka huyo”Alisema Stamina.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here