SHARE

MILAN, Italia

USHINDI dhidi ya Shakhtar Donetsk umemfanya straika wa Inter Milan, Lautaro Martinez, aamini watalinyakua taji la Ligi ya Europa msimu huu.

Martinez na Romelu Lukaku, kila mmoja alifunga mawili na kuiwezesha Inter kuisambaratisha Shakhtar Donetsk kwa mabao 5-0 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa juzi.

Huku Danilo D’Ambrosio naye akifunga siku hiyo, Inter waliingia fainali ya michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010 na watakutana na Sevilla Ijumaa ya wiki hii.

“Tunazidi kuwa moto kutoka mechi moja kwenda nyingi na nafurahia pia kiwango nilichoonesha…” alisema Muargentina huyo aliyesema mabao mawili yake ni zawadi kwa mkewe anayetarajiwa kujifungua.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here