SHARE

NA JESSCA NANGAWE

MWANADADA kutoka kiwanda cha Bongofleva Maua Sama yupo kwenye hatua za mwisho za kumaliza mjengo wake unaodaiwa kutumia mamilioni ya pesa.

Mrembo huyo ambaye mara nyingi amekua hapendi kuonyesha mali anazomiliki inadaiwa kuwa mjengo huyo umemalizika kwa asilimia 90 na wakati wowote huenda akahamia.

Akizungumza na DIMBA Jumatano,Maua Sama hakutaka kuweka wazi hilo lakini akasisitiza kutokana na matunda ya kazi zake ni lazima afanye mambo makubwa ambayo yanaendana na muziki wake.

“Si sawa kusema kwa sasa lakini kama msanii ni lazima nifanye vitu vizuri ambavyo vinaendana na kazi yangu, napenda maendeleo na si nyumba tu yapo mengi yanaendelea na ni mapema kuanza kuyaweka wazi”alisema Maua Sama.

Inadaiwa mjengo huo upo maeneo ya Kigamboni jijini Dar es salaam na hii inakua ni mwendelezo wa mijengo mbalimbali ambayo imekua ikijengwa na mastaa mbalimbali kwa miaka ya hivi karibuni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here