SHARE

NA JESSCA NANGAWE

MKALI kutoka lebo ya WCB Mbosso amefunguka kitu ambacho kiliwahi kumkera zaidi na kumwaribia siku hadi kushindwa kula chakula.

Akizungumza na DIMBA,Mbosso alisema,licha ya kupitia changamoto nyingi kwenye kazi yake ya sanaa lakini siku alipofiwa na mzazi mwenzake Martha na watu kuamini amekwenda msibani kutafuta kiki ni kitu ambacho hawezi kukisahau maishani.

Ukweli kuna mambo mengi nimepitia lakini hili la kuambiwa nimekwenda kwenye msiba wa Martha kutafuta kiki aisee siwezi kusahau, niliumia sana na iyo siku nilishindwa hadi kula chakula, watu walishindwa kutambua ni uchungu gani nilikua nao kwa msiba ule alisema Mbosso.

Hata hivyo Mbosso amekiri kuwa tangu msiba wa mzazi mwenzake utokee bado ni kitu ambacho kimeendelea kumtesa hasa pale anapopata nafasi ya kuonana na mtoto aliyezaa na marehemu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here