SHARE

NA WINFRIDA MTOI

STRAIKA wa Kagera Sugar, Yusuf Mhilu, amezidi kumpa homa, Meddie Kagere wa Simba katika mbio za ufungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Katika orodha ya wafungaji, Kagere ndiye kinara akifunga mabao 19, Mhilu anafuatia na 13 mwingine ni Reliants Lusajo mabao 12.

Hadi ligi ilipofikia inaonekana wazi nyota hao watatu ndio wanaochuana vikali, huku Mhilu akiongoza kufunga tangu kurejea kwa ligi hiyo iliyosimama kutokana na janga la virusi vya corona.

Ukiangalia katika mechi zilizochezwa tangu kurejea kwa ligi hiyo, Kagere hajafunga bao hata moja, huku Mhilu akifunga mawili na Lusajo moja.

Kitendo cha straika huyo zao la Yanga kuingia na kasi ya pekee, kinampa presha Kagere ambaye anatakiwa kufanya kazi ya ziada kuhakikisha anarejea katika ubora wake wa kufumania nyavu. Mara ya mwisho Kagere kufunga ilikuwa Machi 11 mwaka huu walipokutana na Singida United, Simba ikashinda 8-0 huku Mnyarwanda huyo akitupia mabao manne.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here