SHARE

NA MAREGESI NYAMAKA

JUKWAA alilosimama Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa kuwakabidhi Azam Kombe la Shirikiso la Azam(ASFC) uwanja wa Ilulu, Lindi ndilo hilo hilo lililotumika kumtangaza Agrey Morris mchezaji bora wa mashindano.

Aggrey na mwenye miaka 35 amekua chachu ya Azam kurejea kwenye michuano ya Kimataifa kucheza Kombe la Shirikisho barani Afrika msimu ujao.Anaheshimika sana mahali hapo kuanzia wachezaji wenzake, benchi la ufundi, uongozi hadi wafagizi.

Nakukumbusha tu siku moja kabla kocha wake mwenye leseni nzuri ya ukocha ëCV) imejaa kweli kweli, Meja Minganga alikuwa amemtaja huyo huyo Morris kama ni mchezaji wake bora kwa msimu Ligi Kuu Bara.

Ni mtulivu sana.Miguu yake inafanya kazi sana uwanjani kuliko kumlalamikia mwamuzi wala kuwafokea wenzake. Kitambaa kimekaa mahali pake. Yeye na Salum Abubakar ëSure Boyí ndo wenye Azam yao.

Kwa nini Agrey si Obrey Chirwa, Donald Ngoma ambao wamefunga mabao ya kutosha kuliko mchezaji yeyote kikosini hapo? Agrey mbali na kutimiza majukumu yake ana ushawishi kwa wachezaji wenzake. Anajua kucheza mechi kubwa.

Baada ya kuondoka John Bocco, yeye amekuwa ni Azam na Azam ni yeye. Rafiki yake wake wa karibu,Sure boy kuna siku ataanzia benchi kulingana na mahitaji ya kocha kulingana na mchezo husika idara ya kiungo, lakini si Agrey.

Msimu huu alicheza na Abdallah Kheri ëSeboí, Yakub Mohamed kwa uelewano mkubwa katika michuano hiyo kila hatua waliyofuzu ukuta ulikuwa mgumu zaidi kupitika.Mechi mbili mbili za mwisho nusu fainali na fainali yenyewe hawakuruhusu bao.

Kazi ya miguu ya Agrey kwa muda wote hadi sasa, mbele ya viongozi amekuwa kama mboni zao za macho. Ni rahisi tu wasingependa kumpoteza kama ilivyokuwa kwa John Bocco, Aishi Manula na Erasto Nyoni.

Zile faulo huko nyuma alizowachezea kina Emmanuel Okwi (Simba),

Abasirim Chidiebere (Stand Unite) bado hazimuondolei thamani yake. Sergio Ramos wa Real Madrid ameonyeshwa kadi nyingi nyekundu kuliko yeye.

Kinachofanywa na Agrey kutimiza majukumu yake kwa asilimia 100 ni tofauti na weledi eneo la utawala. Si kwamba wachezaji hawapati sitahiki zao kwa wakati? Hapana maamuzi yanapishana kwenda katika benchi la ufundi.

Presha ya matokeo imekuwa kubwa sana. Subira ya kile kilichopangwa awali wakati msimu unaanza mara kadhaa kinaashia katikati ligi ikiendelea. Timu ikitoka sare mbili mfulizo kuna mtu atawindwa.

Misingi ya hatua kwa hatua haipewi nafasi. Nani anajua cheo cha Philipe Alando pale katika benchi siku hizi? Unaambiwa ni mratibu kama Hafidh Saleh pale Yanga.

Tatizo kubwa lilianzia kwa kiongozi wa ngzi ya juu kumsikiliza zaidi rafiki wake wa karibu kuliko maneno yatokayo kinywani kwa mfungaji bora wa muda klabuni, John Bocco.

Nafasi ya juu kabisa ya Mkurugenzi Mtendaji Mkuu ambayo ni daraja la kati ya bodi na benchi la ufundi ufanisi wake ukoje? Aliyewahi kuwa Mwenyekiti, Idrissa Nassor ëFatherí ana kazi kubwa. Kuna kujifunza kutokana na makosa halafu kuna kuamini unachokiamini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here