SHARE

NA JESSCA NANGAWE


NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Linah Sanga, amesema yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha mjengo wake ambao umemgharimu mamilioni ya pesa hadi kufikia hapo.

Linah ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwaye Tracyparis, alisema kitu kikubwa anachojivunia kwa sasa ni kuona nyumba yake ya kisasa ikiwa hatua za mwisho kukamilika.

“Nashukuru Mungu kwa sasa nyumba yangu imefikia hatua nzuri na kwa uwezo wake itakamilika wakati wowote, nimetumia pesa nyingi lakini yote ni matunda ya kazi zangu,” alisema Linah.

Linah kwa sasa ameachia ngoma mpya inayojulikana kwa jina la Koleza ambayo inafanya vyema kwenye vituo mbalimbali vya redio.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here