SHARE

NA JESSCA NANGAWE
UPO uwezekano mkubwa kiungo wa kimataifa wa Simba, Mghana Bernard Morrison aukosa mchezo wa ëKariakoo Derbyí unaotarajiwa kupigwa Novemba 7 dhidi ya watani zao wa jadi Yanga.

Hatihati ya Morrison kuukosa mchezo huo imekuja siku moja baada kufanya tukio la kumtwanga beki wa Ruvu Shooting, Juma Nyoso katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Jumatatu wiki hii.

Kanuni ya 39 (5)(5.2) inaeleza mchezaji yeyote atayepigana kabla ya mchezo au baada ya mchezo kumalizika atafungiwa michezo isiyopungua mitatu na kulimwa faini isiyopungua sh. 500,000.
Pia Kanuni ya 39(6) mchezaji atayebainika kukutwa na makosa ya utovu wa nidhamu yanayojirudia mara nyingi atafungiwa kucheza kati ya michezo 5 mpaka 10 na faini isiyopungua shilingi milioni 1.

Hivyo basi kutokana na kanuni hizo kama zitafuatwa kama zilivyo basi ni wazi kuwa Morrison ataikosa Yanga kwa kuwa kanuni ya 35 inasema atafungiwa michezo 3 ambapo Simba imebakisha michezo miwili kabla ya kukutana na Yanga.
Kwenye mchezo Simba na Ruvu Shooting, Morrison alionekana akimpiga ngumi Nyoso baada ya mechi kusimama dakika ya 72 kutokana na kutokea kwa vurugu.
Vurugu hizo zilisababishwa na wachezaji wa Ruvu Shooting kugomea penalti waliyopewa Simba na ilipigwa na John Bocco ambaye alikosa.

Kutokana na vurugu hizo mchezaji wa Ruvu Shooting, Shaaban Msala alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na mwamuzi wa kati ingawa Morrison hakuonyeshwa kadi kwa kile ambacho ilionekana mwamuzi hajaona tukio hilo lililorushwa moja kwa moja na Azam Tv.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here