SHARE

MANCHESTER, England

BAADA ya kipindi kifupi cha matokeo ya kukera ndani ya klabu yake ya Manchester United, kocha Jose Mourinho, amedhamiria kuanza na safisha safisha ya wachezaji mara baada ya dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa Januari mwakani.

‘Red Devils’ hao wameshinda michezo miwili tu kati ya saba ya mwisho katika michuano yote, matokeo yaliyomfanya Mourinho asiwe na furaha.

Kwa mujibu wa taarifa za mtandao wa Telegraph, Mourinho anataka kupunguza wachezaji wanane ndani ya kikosi chake, iwe ni Januari au kipindi cha majira ya kiangazi mwaka 2017.

Orodha hiyo imewajumuisha Matteo Darmian, Marcos Rojo, Phil Jones, Bastian Schweinsteiger, Morgan Schneiderlin, Michael Carrick, Memphis Depay na Ashley Young.

Kulingana na maelekezo yaliyopo kwenye mikataba yao, fagio hilo halitakuwa rahisi kama inavyofikiriwa lakini klabu ina matumaini ya kukamilisha uhamisho au kuvunja baadhi ya mikataba ya wachezaji hao.

Mtandao wa The Sun nao ulitoa taarifa kwamba United itahitaji kiasi cha euro milioni 11 ili kumwachia kiungo wao Mjerumani, Schweinsteiger.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here