SHARE

Arsenal ya Pochettino ‘kiboko ya uchafu’ EPL

LONDON, England

ZILEkeleleza mashabikiwa Arsenal kutaka Unai Emery aondoke, zilizaa matunda juzi, ambapo Mhispania huyo alitimuliwa saa chache baada ya Washika Bunduki hao kulazwa 2-1 na Frankfurt ya Ujerumani katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Europa.

Miezi 18 pekee tangu alipopewa kazi, Emery alikuwa kwenye wakati mgumu katika wiki za hivi karibuni kwani mchezo dhidi ya Frankfurt ulikuwa wa saba mfululizo bila kikosi chake kuvuna ushindi.

Mkongwe wa timu hiyo, Freddie Ljungberg, amekalia kwa muda kiti cha kocha huyo, huku Mauricio Pochettino akiwa kinara katika wale wanaoweza kutangazwa, ingawa pia kuna majina ya Nuno Espirito Santo wa Wolves na Carlo Ancelloti anayeinoa Napoli.

Pochettino aliyefukuzwa Tottenham anapewa nafasi kubwa kutokana na sababu mbalimbali, kubwa ikiwa ni uzoefu wa miaka mitano katika mikikimikiki ya Ligi Kuu ya England (EPL), huku suala la kumaliza ndani ya top four likiwa la kawaida kwake, tofauti na Arsenal katika miaka ya hivi karibuni.

Je, mashabiki watarajie kuiona Arsenal ya aina gani chini ya Pochettino, ikizingatiwa kuwa atahitaji kukifanyia marekebisho makubwa kikosi hicho katika dirisha la usajili la Januari, mwakani?

Ukianza na eneo la beki wa kati, David Luiz aliyetokea Chelsea haonekani kuwa msaada mkubwa, hivyo ni wazi Pochettino atamfuata kwa mara nyingine Daniele Rugan aliyemkosa akiwa kocha wa Tottenham.

Kazi haitakuwa ngumu safari hii kwani tayari Arsenal walishaanza kumfukuzia staa huyo wa Juventus, ikiwa haijasahaulika kuwa klabu hiyo ya Serie A iligoma kumwachia kwa mkopo miezi minne iliyopita.

Safu ya kiungo ya Pochettino pale Arsenal nayo inatarajiwa kupitia maboresho, hasa kwa kuwa kiwango cha Granit Xhaka si cha kutabirika. Hapo Pochettino anatarajiwa kumfuata Thomas Partey wa Tottenham kwa kuwa ni mchezaji aliyeanza kumtamani na kumnyatia tangu akiwa Tottenham.

Kocha huyo ni shabiki mkubwa wa Partey raia wa Ghana na alianza kuvutiwa naye baada ya nyota huyo kuonesha kiwango cha juu katika moja ya michezo kati ya Atletico na Real Madrid.

Katika eneo la ushambuliaji, ni kweli Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette wamekuwa wakifanya vizuri lakini Nicolas Pepe amefeli, licha ya kununuliwa kwa mkwanja wa maana akitokea Lille.

Ili kuliongezea makali eneo hilo, ni wazi Pochettino atajisogeze kwa Hakim Ziyech wa Ajax aliyemtaka wakati Tottenham. Kama itashindikana, basi haitashangaza kwa mashabiki wa Arsenal kumuona Memphis Depay akisogea Emirates kwani naye ni sehemu ya washambuliaji aliojaribu kuwasajili akiwa Tottenham.

Pia, kwa upande wa pembeni, Arsenal wamekuwa wakimfukuzia kwa muda mrefu na hata kabla ya kuondoka juzi, Emery alikuwa akimtaja kati ya wale anaowataka hapo Januari, mwakani.

Tayari Pochettino anazikuta Pauni milioni 80 alizokuwa ameomba Emery ili amsajili Zaha, ambaye alijaribu kumvuta Tottenham katika usajili wa kiangazi, mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here