SHARE

Na MOHAMED KASSARA

MCHAMBUZI maarufu wa soka nchini , Alex Kashasha amefichua siri ya vipigo wanavyokutana navyo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara,Simba kuwa vinatokana na kikosi hicho kucheza kwa staili moja licha ya kukutana na wapinzani tofauti.
Kauli hiyo imekuja baada Simba kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa juzi katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kipigo hicho kilikuwa cha pili mfululizo kwa Wekundu hao wa Msimbazi ambao ndiyo mabingwa watetezi wa ligi hiyo baada ya kutoka kupata matokeo kama hayo katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga.
Kashasha alisema, hayo wakati akitoa uchambuzi wake baada ya mchezo huo kukamilika ambapo alifafanua kwamba Simba ilistahili kushinda mchezo huo, lakini kilichowaangusha nikushindwa kuwa na mpango mbadala.
ì Ninachokiona mimi kwenye hizi timu zetu sitazitaja lazima uwe na culture(tamaduni) au philosophy (falsafa) zaidi ya mbili kwenye kuifundisha timu, Simba ilikua na kila sababu ya kushinda huu mchezo kwa sababu ina wachezaji wengi wazuri lakini tatizo kubwa wanacheza staili ileile moja,alisema Kashasha.

SHARE
Previous articleMORRISON HATIHATI KUIVAA YANGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here