SHARE

NA WINFRIDA MTOI

KOCHA mpya wa Yanga, Mbelgiji Luc Eymael, amekuja na staili yake ya mazoezi katika kikosi hicho tofauti na ilivyozoeleka.

Siku ya kwanza tu kutua mazoezini, Eymael alihakikisha  anakuwa na mipira ya kutosha na vifaa vyote vinavyohitajika kufanyia mazoezi kwa wachezaji.

Hali hiyo iliwafanya viongozi wa Yanga, kuingia dukani fasta na kuleta vifaa vilivyokosekana na kuongeza mipira mipya.

Baada ya kuridhika, aliingia uwanjani na shughuli ikaanza licha kuwa siku ya kwanza, aliwafanyisha wachezaji mazoezi ya maana, akihakikisha kila mmoja anafuata kile anachokitaka.

Wachezaji waliompagawisha zaidi miongoni mwao alikuwa straika Ditram Nchimbi, aliyemudu kasi ya  kocha huyo aliyetaka mchezaji kuwa  makini anapofika katika eneo la goli.

Nchimbi ni kati ya wachezaji walioonekana kwenda sambamba na kocha huyo, akifanikiwa kupiga mashuti mazuri yanayolenga lango na  kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi  katika siku ya kwanza.

Katika dakika chache walizokuwa wanaelekezwa jinsi ya kupiga mashuti yenye faida, Nchimbi alifanikiwa kutumbukiza nyavuni zaidi ya mabao matano.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here