SHARE

NA JESSCA NANGAWE

MWANADADA kutoka kiwanda cha Bongofleva Rose Ndauka amefunguka kuwa furaha yake kwa sasa nikuona anakwenda kuitumikia ndoa yake kikamilifu na kuwa mke wa mfano.

Ndauka ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwaye Barveen alifunga ndoa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es salaam.

Akizungumza na DIMBA Jumatano,Ndauka amekiri kuwa ndoa za mastaa wengi zimekua zikikumbwa na changamoto nyingi jambo ambalo mara nyingi halizuiliki lakini anatamani yake iwe ya mfano.

“Changamoto zipo na hazizuiliki,kikubwa namuomba Mungu anisaidie,pia nitahakikisha nakuwa mfano wa kuigwa kwa mastaawengine”alisema Ndauka.

Alisema,anashukuru kuona moja ya ndoto zake za kuitwa mke zimetimia na kilichobaki ni kutunza jina lake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here