SHARE

BEIJING, China


NYOTA wa zamani wa Chelsea, Oscar, huenda akaonekana na uzi wa timu ya taifa ya China katika siku za usoni.

Mbrazil huyo, licha ya kuichezea nchi yake mechi 47, hajaitwa tena tangu mwaka 2015, hivyo sasa anafikiria kutinga jezi za China.

Oscar mwenye umri wa miaka 28, alijiunga na Shanghai SIPG ya China mwaka 2016 na atakuwa ametimiza vigezo vya kupata uraia wa China hapo mwakani.

Licha ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kuzuia mchezaji kubadili timu ya taifa akiwa ameshaichezea nyingine, Oscar alisema yuko tayari kuhamia China endapo sheria hiyo itabadilishwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here