SHARE

LONDON, England

ARSENAL wameripotiwa kuwa na mpango wa kuachana na nyota wake, Mesut Ozil, kipindi cha usajili wa kiangazi, mwaka huu.

Akiwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake, Ozil amefunga bao moja pekee na kutoa asisti mbili na hakucheza wakati Arsenal ikitandikwa mabao 3-0 na Manchester City.

Sasa, kwa mujibu wa vyombo vya habari, Ozil atakatwa ili kupunguza mzigo wa mshahara mnono anaopokea, Pauni 350,000 (zaidi ya Sh mil 990 za Tanzania).

Kwa upande mwingine, zipo taarifa zinazodai kuwa Ozil anataka kubaki Emirates na kupigania namba kwenye kikosi cha Washika Bunduki hao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here