SHARE
NEWARK, NEW JERSEY - AUGUST 26: Rapper Rick Ross attends the 2019 MTV Video Music Awards red carpet at Prudential Center on August 26, 2019 in Newark, New Jersey. (Photo by Aaron J. Thornton/Getty Images)

MIAMI, Marekani

MOJA kati ya Marapa wenye majina makubwa nchini Marekani ni William Leonard Roberts II, Rick Ross, aliyezaliwa katika kitongoji cha Clarksdale, Mississippi, lakini akikulia zaidi katika viunga vya Carol City, Florida nchini Marekani.
Mkali huyo aliyezaliwa Januari 28, 1976 hivi sasa akiwa na miaka 44 alipata elimu yake katika shule ya Miami Carol City Senior High School na kuendelea na elimu ya chuo katika chuo cha watu weusi cha Albany State University ambapo alipata nafasi hiyo kutokana na uwezo wake wa kucheza soka.
Mara baada ya kumaliza Roberts aliwahi kufanya kazi ya ukusanyaji data kwa miezi 18 kutoka Disemba 1995, hadi alipoamua kuacha Juni 1997.
Alipoacha kazi aliingia moja kwa moja katika kazi ya muziki katika studio za Suave House Records, huku akijiita Teflon Da Don, nyimbo yake ya kwanza aliipa jina la “Ain’t Shhh to Discuss” ambayo ilikuwa katika albamu ya Erick Sermon iliyofanywa na DreamWorks.
Mwanzo mwa mwaka 2000 alibadili jina kutoka Teflon da Don akichukua jina la muuza madawa ya kulevya hatari ambaye alikuwa akiogopeka kipindi hicho alikuwa kifungoni kwa wakati huo jambo lililosababisha kuwepo na maswali mengi kwa nini aliamua kuchagua jina hilo.
Yafuatayo ni mambo matano ya ndani yanayomuhusu mkali huyo wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani ambaye kwa muda mrefu amekuwa kwenye chati.
Ana jumla ya tattoo 500 mwilini
Nyota huyo wa vibao vikali kama vile Hustling, Am Sorry na vingine vingi ni mpenzi mkubwa wa Tattoo ambapo alianza kuchora akiwa na miaka 13 ambapo hadi sasa amefikisha jumla ya tattoo 500 mwilini mwake.
Aliwahi kuwa mwanasoka
Watu wengi hasa wapenzi wa muziki wa kufoka, Hip Hop wamemjua mkali huyo kupitia muziki lakini nyuma ya kipaji hicho nyota huyo pia aliwahi kuwa hatari pia katika mchezo wa soka alipokuwa akisoma katika shule ya Miami Carol City Senior High School.

Ni msomi mzuri wa biblia
Wasanii wengi wamekuwa wapenda starehe huku wakificha mambo yao ya kiimani hali ni tofauti kwa Rick ambaye ameweka wazi kuwa yeye ni msomi mzuri wa kitabu kitakatifu Biblia na hupendelea zaidi kusoma Zaburi ya 27:1-4.

Ni muongozaji wa filamu
Mbali na mchezo wa soka pamoja na kipaji chake maridhawa cha muziki kilichomtambulisha ulimwenguni kote Rick Ross pia ni mkali mwenye uwezo wa kuongoza filamu kazi ambayo amesema anatamani zaidi kuifanya atakapokuwa amepumzika kufanya muziki.

Hulala saa mbili kulala
Huenda ikawa ni ajabu lakini kweli Rick Ross, anasema hutumia saa mbili hadi tatu kuupumzisha mwili wake, muda ambao ni mchache zaidi kitaalamu ambapo inashauriwa mtu anapaswa kupumzika kwa saa sita ili kuufanya mwili ukae sawa jambo ambalo ni kinyume kwa rapa huyo.

SHARE
Previous articleWolper aipa kisogo Valentine Day
Next articlePATANOGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here