SHARE

NA MARTIN MAZUGWA

TIMU ya Ruvu Shooting watawakosa wachezaji wao watatu katika mchezo wao wa Ligi Kuu mwishoni mwa wiki hii dhidi ya Ndanda FC kutokana na majeraha yanayowakabili.

Akizungumza na DIMBA jana, Msemaji wa timu hiyo, Masau Bwire, amesema hali hiyo inampa wakati mgumu kocha kukiandaa kikosi chake kuelekea kwenye mchezo huo dhidi ya Ndanda FC.

“Ni kweli tunao wachezaji wetu ambao ni majeruhi hali ambayo inampa wakati mgumu kocha wetu, hata hivyo Ruvu Shooting inao wachezaji wengi ambao wanaweza kuziba nafasi zao,” alisema Bwire.

Wachezaji ambao watakosekana katika mchezo huo ni pamoja na Richard Peter anayesumbuliwa na nyama za paja, Mao Bofu, anayesumbuliwa na enka huku Sunday Magwaja anasumbuliwa na misuli.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here