SHARE

NA TIMA SIKILO

UNAAMBIWA huko Azam FC wameanza kuingiwa na presha baada ya straika wao mahiri Obrey Chirwa, kukataa kuongeza mkataba mpya huku akihusishwa kutakiwa na Simba.

Mkataba wa Chirwa na Azam unafikia tamati mwishoni mwa msimu huu lakini inadaiwa kila akiitwa mezani anagoma kuongeza mkataba mpya kama ilivyo kwa mwenzake Donald Ngoma.

Kigogo mmoja wa Azam FC, ameliambia DIMBA Jumatano kuwa, Chirwa hataki kuongeza mkataba mpya licha ya uongozi kumuhakikishia mshahara mzuri.

“Tunataka kuendelea kuwa naye lakini hataki kuongeza mkataba mpya, hatujui ana malengo gani kwani baadhi ya wenzake akiwamo Donald Ngoma, tumeshawaongezea mikataba mipya,” alisema kigogo huyo.

Taarifa nyingine zinadai kuwa, straika huyo anawindwa na Simba kwa kila hali ili kuongeza nguvu kwa Wekundu hao wa Msimbazi ambao wanatarajia kuiwakilisha tena nchi michuano ya kimataifa kama watatetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Bara.

Chirwa ambaye aliichezea Yanga kwa mafanikio, ameichezea Azam msimu huu na inasemekana huenda akatimkia Simba baada ya kushawishiwa na mabosi wa Wekundu hao wa Msimbazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here