SHARE

NA JESSCA NANGAWE

WAWAKILISHI wa klabu ya Waasland Bareven ya nchini Ubelgiji tayari wametua nchini kwa ajili ya kukutana na uongozi wa Yanga kufanya mazungumzo ya kumuuza straika wao wa Kimataifa Heritier Makambo.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Frederick Mwakalebela, ameliambia DIMBA Jumatano kuwa ni kweli Wakala wa mchezaji huyo amewasili jana na huenda leo wakafanya naye mazungumzo kuhusu kiasi cha pesa wanachohitaji ili kumtoa mshambuliaji huyo tegemeo wa klabu hiyo.

“Ni kweli wakala wa wachezaji wa klabu ya Bareven amewasili nchini na tumewasiliana nae, kilichopo tutafanya mazungumzo na kasha kutangaza tulipofikia kuhusu kuuzwa kwa Makambo”Alisema Mwakalebela.

Imeelezwa kuwa klabu hiyo imetenga kiasi kikubwa cha pesa ili kupata huduma ya straika huyo na kuhakikisha inaingia vitani ili kuweza kumsajili Makambo.

Kwa mujibu wa wakala wa kusaka vipaji wa klabu hiyo Raoul Alfred alisema ni kweli wamekuja kwa lengo la kuzungumza na Yanga juu ya kumnunua mchezaji huyo kutokana na kuhitaji huduma yake ndani ya klabu yao.

Mbali ya klabu hiyo Makambo pia alihusishwa kuhitajiwa na klabu ya Horoya AC ya Guinea ambayo tayari ilimfanyia vipimo vya afya wiki iliyopita lakini hawakuweza kufikia muafaka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here