SHARE

                      Lulu Ringo, Dar es Salaam

Mshambuliaji kinda wa klabu ya Simba Adam Salamba amesema ndoto yake kubwa ni kuiwakilisha Tanzania kimataifa kupitia timu ya Taifa, (Taifa Stars).

Salamba ambae amesajiliwa na Simba mwanzoni mwa msimu huu akitokea Mkoani Iringa katika timu ya Lipuli (Wanapaluhengo) amesema anatami siku moja kuwa mmoja kati ya wachezaji watakao peperusha bendera ya Tanzania vizuri katika mashindano mbalimbali ambayo timu hiyo itakua inashiriki.

“Licha ya kuwa mchezaji wa Simba,  ndoto yangu kubwa ni siku moja kuiwakilisha nchi yangu katika mataifa mbalimbali,  kwasasa najituma kwa nguvu zangu zote ili kuwaonyesha walimu wa timu ya taifa uwezo nilio nao, naamini ipo siku ndoto zangu zitakua kweli,” amesema Salamba.

Licha ya kinda huyo kuitamani Stars,  awali ndoto zake zilikua kuzichezea Simba na Yanga vilabu vyenye ushindani zaidi katika ligi kuu ya Tanzania Bara, ndoto yake ilitimia baada ya kusajiliwa katika klabu ya Simba, usajili uliotikisa baada ya Kinda huyo kusajiliwa kwa pesa ndefu akitokea Lipuli.

Aidha Salamba ameweka wazi kuvutiwa na Mchezaji wa kimataifa anaekipiga nchini Ubelgiji katika timu ya KRC Genk, Mbwana Samatta na kusema anatamani siku moja kuja kuwa kama yeye.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here