NA JESSCA NANGAWE
KUNDI la muziki Sauti Sol kutoka nchini Kenya amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha aliyekua Rais wa Awamu ya Tatu nchini Tanzania, Benjamin William Mkapa.
Kifo cha kiongozi huyo wa zamani, kilitokea usiku wa Ijumaa hii jijini Dar es salaam baada ya kuugua na kulazwa hospitalini.
Kupitia akaunti yao ya Twitter kundi hilo lilimweleza kiongozi huyo kama miongoni mwa marais wa Afrika walioweza kufanya mambo makubwa katika uongozi wake.
“Ni msiba wetu sote lakini sala zetu tunazielekeza kwa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania katika kipindi hiki kigumu wanachokipitia,”ulieleza ujumbe huo.
Rais wa Tanzania John Magufuli ametangaza siku saba za maombolezo kufuatia kifo hicho huku Uwanja wa Uhuru ukiteuliwa kutumika katika shughuli za kumuaga kiongozi huyo.