SHARE

CATALUNYA, Hispania

SULUHU ya juzi dhidi ya Sevilla yalimzuia Lionel Messi kufikisha mabao 700 tangu aanze kucheza soka la kulipwa.

Wakati huo huo, yameiweka pabaya Barcelona kwani endapo Real Madrid wataifunga Real Sociedad leo, basi timu hizo zitakuwa sawa kwa pointi.

Hivyo basi, Messi anapaswa kusubiri hadi Jumanne ya wiki ijayo kuona kama atafunga dhidi ya Athletic Bilbao kufikisha idadi hiyo ya mabao inayojumuhisha ngazi ya klabu na timu ya taifa.

Katika mchezo mwingine, Villarreal walijiimarisha katika nafasi yao ya kusaka tiketi ya Ligi ya Europa kwa kuibanjua Granada bao 1-0.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here