SHARE

NA JESSC NANGAWE

WAKATI rapa wa Marekani akifanya shoo ya aina yake katika nchi za Nigeria na Ghana, msanii Gift Starnford Gigy Money amekiri kuwa rapa huyo amekua akimnyima usingizi kwa mafanikio anayoyapata.

Hivi karibuni rapa huyo alizua gumzo nchini Nigeria na Ghana ambapo alialikwa katika shoo huku akiingiza zaidi ya bilioni 3 za kitanzania kupitia shoo hizo.

Akizungumza Gigy Money alisema, mafanikio ya rapa huyo wa kike yamekua chachu kwake ya kuendelea kujituma zaidi kupitia kazi zake na kudai kuna wakati utafika way eye kurithi mafanikio yake.

ìNi kweli Card B anastahili kupata mkwanja kama huo, kwanza kwangu namuona ni mwanamke mwenye uthubutu, anajiamini na hata ukiangalia baadhi ya shoo zake amekua anafanya kwa kujituma na kutambua yupo kazini, hivyo ndio wanawake tunapaswa kuwaîalisema Gigy Money.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here