SHARE

MANCHESTER, England 

DAVID Silva yupo kwenye mazungumzo kurudi katika klabu yake ya zamani ya Valencia lakini dili hilo linakwamishwa na janga la virusi vya corona.

Silva aliweka wazi nia yake ya kuondoka Manchester City mwishoni mwa mkataba wake ambayo inamalizika Juni 30 mwaka huu. 

Valencia wameonyesha nia ya kumsajili tena kiungo huyo Mhispania miaka 10 baada ya kuondoka Uwanja wa Etihad lakini mazungumzo yamekwamishwa na hatima ya covid-19 kwa wachezaji ambayo mikataba yao inamalizika msimu huu.

FIFA imependekeza mikataba inayomalizika June 30 kuongezwa hadi msimu unapomalizika lakini wazo hilo limezua jambo kwa mabosi wa Ligi Kuu England wakisema itakuwa vigumu kutekelezeka kisheria.

Watu wa ndani wameliambia ESPN kuwa Silva, aliyetimiza miaka 34 Januari, ama atakubaliana mkataba wa muda mfupi kubaki Man City au aondoke June 30. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here