SHARE

Hahaha wakati mwingine unaweza ukacheka ukisikia ubishi unaoendelea mitaani, ukweli naanza kuamini kwamba ukitaka kua mwenye furaha kila siku uwe shabiki wa soka.

angalia leo ubishi uliofika kijiweni kwetu, unadhani kama huna habari na masuala ya mchezo huu, utaambulia nini zaidi ya kununanuna tu.

leo bwana kilicholetwa mimi kama mwenyekiti sina haja ya kupoteza muda, hebu niwaachie wenyewe waweke mada mezani kisha waanze kutupa mistari.

simba day

jamani tuache masihara, mtu aliyeumiza kichwa na kubuni hili tamasha la siku ya simba almaarufu simba day, anastahili pongezi.

binafsi nampongeza mwenyekiti wa zamani wa simba, hassan dalali, kwa ubunifu huu.

halafu nichukue nafasi hii kuwapa ukweli mashabiki wote wa soka, kwamba mpango huu japokuwa umebuniwa na simba, si vibaya kuiga.

siku ya simba ina raha naweza kusema kuliko hata baadhi ya sikukuu, watu wanakutana wanapendeza kwa mavazi ya rangi zao, lakini kubwa zaidi kutakuwa na burudani kali ya soka.

yapo matamasha yaliyowahi kufanyika sehemu mbalimbali lakini hili nasema ni bab’ kubwa na katika medani ya soka, sioni kama kuna kinachokutanisha wadau wengi kama simba day.

namalizia kwa kuwaalika washkaji hata kama sio simba na japokuwa mimi mwenyewe sina ushabiki wa timu hizi mbili yani simba wala yanga, lakini hili nawapa big up, simba day ndio mpango mzima.

ngao ya jamii

huyu dogo hawezi kubisha kama yeye si shabiki wa simba, maana huo ufagio si wa nchi hii na mimi niseme tu kwamba yeye ameleta mada hii akiwa na nia tu ya kuwafagilia hao simba.

lakini nikaona nisibishane naye ila tu nimkumbushe aina ya mechi nyingine zinazovuta hisia za watu wengi.

maana naona dogo amejisahau hata akashindwa kuzitaja mechi zinazokutanisha simba na yanga na nyingine kibao za aina hiyo.

sioni aibu hata kumkumbusha kwamba mwaka huu michuano ya ndondo cup nayo pia ilikusanya watu pengine hata huko taifa hawatajaa simba kama anavyotufunga kamba za katani.

lakini nataka nimkumbushe tu kwamba, kinachoendelea hivi karibuni baada ya kufaglia tamasha lake la simba day, asikose kuja kuangalia pambano la ngao ya jamii litakaloashiria kufunguliwa kwa michuano ya ligi kuu.

hapa ataona sura za furaha kwa pande zote, awataona yanga, azam, mtibwa na mashabiki wengine mbalimbali.

kwenye furaha za kuchanganyika ndiyo kwenye raha achilia mbali siku hiyo rangi zitafanana na hata kushangilia kwenyewe mpira zitakuwa sauti za aina moja.

hata ndege huimba kwa sauti wakipishana ndipo huleta ladha ya wimbo, tuache ushabiki, tuzungumzie ukweli ndiyo raha ya kijiwe hiki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here