SHARE

NA EZEKIEL TENDWA

UONGOZI wa Klabu ya Simba umesema maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wao wa Bunju yanakwenda vizuri na wanatarajia kuuzindua kwenye wiki ya Simba Day.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Crescentius Magori, alisema mambo ni mazuri katika zoezi la Uwanja huo na kila kitu kitakuwa sawa siku chache zijazo.

“Ujezi wa viwanja vyetu Bunju unaendelea, nafurahi kwamba wiki ya Simba Day tutakwenda kuweka jiwe la msingi kuashiria uzinduaji wa Bunju project.

“ Sasa hivi tuna viwanja viwili vinatengenezwa sambamba, Uwanja wa nyasi bandia na Uwanja wa nyasi za kawaida, katika wiki ya Simba Day, moja ya shamrashamra zetu ni kuzindua Uwanja,” alisema. Simba Day inatarajiwa kufanyia siku ya Alhamis ya Agosti 8 mwaka huu ambapo Magori alisema msimu huu itafana zaidi ya miaka mingine yote iliyopita kutokana na maandalizi wanayoyafanya huku akidai muda wowote wataweka bayana timu watakayoialika kucheza na Wekundu hao wa Msimbazi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here