SHARE

NA DUSTAN SHEKIDELE, MOROGORO

BAADA ya kambi ya wiki mbili mkoani Morogoro, hatimaye Simba jana ilidhihirisha kuwa itakuwa moto wa kuotea mbali msimu ujao baada ya kuwaonyesha hasira Polisi Moro kwa kuwafunga mabao 6-0 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa jana jioni kwenye Uwanja wa Highland, Bigwa, mkoani hapa.

Simba iliyoweka kambi Chuo cha Biblia mjini humo kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ilionekana kupania vilivyo tangu mwanzo wa mchezo ambapo hadi mapumziko wekundu hao tayari walikuwa wamekwishaweka wavuni mabao 2-0 yaliyofungwa na Muivory Coast, Frederick Blagnon dakika ya 10 na 30.

Kipindi cha pili makocha wa timu zote walifanya mabadiliko ambapo Simba ndio walionufaika na mabadiliko hayo ambapo dakika ya 48, lbrahim Ajib alifunga bao la 3.

Ajib tena aliongeza bao la 4 dakika ya 68 na Mohamed Kijiko akafunga bao la 5 dakika ya 77 huku Abdi Banda akimalizia bao la 6 dakika ya 82.

Mashabiki waliofurika katika mchezo huo kwa kiingilio cha bure walionekana kuridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na timu yao na kufufua matumaini ya timu yao kuwapa  raha msimu huu.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa: Vincent Angban, Janvier Besala Bokungu/Hamad Juma, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’/Abdi Banda, Method Mwanjali, Novat Lufunga/Juuko Murushid, Muzamil Yassin, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Said Ndemla, Shizza Kichuya/Mohammed Mussa, Frederick Blagnon/Mussa Mgosi/Peter Mwalyanzi, Ibrahim Hajib/Awadh Juma na Jamal Mnyate/Danny Lyanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here