SHARE

NA EZEKIEL TENDWA

KAMA Mtibwa Sugar wataichukulia mechi yao dhidi ya Simba kesho kimasihara, wanaweza wakaondoka na kapu la mabao kutokana na Wekundu hao wa Msimbazi kukerwa na matokeo waliyoyapata michezo yao miwili iliyopita.

Simba ndio watakaokuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Wekundu hao, wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kushindwa kupata matokeo mazuri katika michezo miwili iliyopita na watataka kumalizia hasira zao kwa Mtibwa Sugar.

Michezo hiyo ni dhidi ya Kagera Sugar, ambapo walikubali kipigo cha bao 1-0 na juzi Jumatatu wakilazimishwa sare ya kutofungana na Azam FC michezo yote ikichezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Licha ya matokeo hayo yasiyoridhisha, kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amewaambia mashabiki wa kikosi hicho wasiwe na wasiwasi kwasababu dhamira ya kutetea ubingwa wao ipo palepale.

“Hatujapata matokeo ya kufurahisha katika michezo miwili dhidi ya Kagera Sugar na Azam lakini hiyo haimaanishi kwamba tumepoteza matumaini ya kutetea ubingwa wetu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here