SHARE

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa wachezaji wa ndani CHAN, pamoja na Kombe la Shirikisho, wapo katika maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kwa michuano hiyo mwezi ujao.

Tanzania itawakilishwa na timu nne, Simba na Yanga zikicheza Ligi ya Mabingwa na KMC na Azam wao wakipamba katika mashindano ya Kombe la Shirikisho.

Kwa sasa Simba ipo nchini Afrika Kusini ilikoweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo pamoja na Ligi Kuu, Yanga nao wakiweka kambi eneo la Bingwa mjini Morogoro.

Azam FC, KMC hivi karibuni zilikuwa nchini Rwanda zikicheza michuano ya Kombe Kagame, huku vigogo Simba na Yanga wakiendelea na mazoezi pamoja na mechi za kirafiki.

Simba jana ilicheza dhidi ya Orbret Tvet na kuiangushia kipigo cha mabao 4-0, Yanga nao wakicheza mechi tatu na kushinda zote.

Sisi Dimba tumeridhishwa na maandalizi ya timu hizi nne, ambazo ndiyo zilizobeba dhamana ya kuwatoa kimasomaso Watanzania katika michuano hiyo ya kikmataifa.

Hata hivyo bado tunashauri timu hizi kuhakikisha zinapata mechi za kirafiki dhidi ya timu zenye viwango vitakavyotosha kuzipima kabla ya kushiriki michuano hiyo inayoshirikisha vigogo vya soka Afrika.

Tunafahamu kuwa timu zetu zitaanza kupata mtihani katika mechi za mwanzoni tu kutokana na ratiba kuzipanga na timu ngumu na zenye uzoefu wa michezo ya kimataifa.

Licha ya Yanga kucheza mechi yake ya kwanza kwa kuivaa Township Rollers ya Botswana, ambayo kihistoria wanaifahamu na Simba kuwafuata UD Do Songo bado kunaleta matumaini, bado zinahitajika mechi za kirafiki dhidi ya timu zenye viwango ili kuweza kupata tathmini ya michezo itakayokuja.

Tunajua kwamba, makocha wanatumia kipindi hiki kuwafahamu wachezaji na kuwapima, lakini ni muhimu wakajua kwamba wachezaji hawa licha ya uwezo wa kila mmoja, lakini wanatakiwa waunganishwe ili wacheze kama timu na hasa katika mechi kubwa kama hizo zinazotajia kuanza mwezi ujao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here